image

Frequent Asked Questions

1. Nywele zangu zinakatika sana, nifanyeje?
Kukatika kwa nywele mara nyingi husababishwa na ukavu, kukosa unyevu, au kutotumia routine sahihi.

Tunashauri uanze routine hii:

🧼 Foaming Nourish Shampoo – Osha mara 1 kwa wiki.

🧴 Deep Nourish Conditioner – Tumia baada ya shampoo kurejesha unyevu.

πŸ’§ Ultra-Moisture Leave-In Conditioner – Tumia kwenye nywele zenye unyevunyevu.

🌿 Hair Growth Oil – Pakaa kwenye ngozi ya kichwa mara 3–4 kwa wiki.

πŸ₯‘ Hair Nourish Butter – Funga unyevu ili nywele zisikauke.

πŸ’¦ Hair Growth Spray – Tumia kila siku kuongeza unyevu.

Ukifuata routine hii kwa uaminifu, utasaidia kupunguza kukatika kwa nywele.


2. Nywele zangu hazikui na zinakatika.
Mara nyingi nywele zinakua, lakini zinakatika kabla hazijafikia urefu unaotaka.

Sababu kuu ni:
β€’ Ukavu wa nywele
β€’ Kukosa unyevu
β€’ Ngozi ya kichwa kutokuwa na afya
β€’ Kutotumia routine sahihi

Routine kamili ya ESN itasaidia kuweka nywele zenye afya, kupunguza kukatika na kuhifadhi urefu wa nywele.


3. Nywele zangu ni kavu na zinakatika.
Nywele za asili huwa na tabia ya kukauka. Zikikosa unyevu, hukatika kwa urahisi.

Tunashauri utumie:
πŸ’¦ Hair Growth Spray kila siku.
πŸ’§ Ultra-Moisture Leave-In Conditioner baada ya wash day.
πŸ₯‘ Hair Nourish Butter kufunga unyevu.
🧴 Deep Nourish Conditioner kila wash day.

Hakikisha hupaki butter kwenye nywele kavu. Tumia kwenye nywele zenye unyevunyevu.


4. Bidhaa za ESN zinafaa kwa watoto?
Ndiyo. Bidhaa za Esther's Secret Naturals zimetengenezwa kwa viambato vya asili na ni laini kwa nywele na ngozi ya kichwa. Zinafaa kwa watoto na watu wazima.

Kwa watoto wadogo, tunashauri kuanza na:
β€’ Foaming Nourish Shampoo
β€’ Deep Nourish Conditioner
β€’ Ultra-Moisture Leave-In Conditioner
β€’ Hair Growth Spray


5. Bidhaa za ESN zinafaa kwa nywele zenye dawa (relaxed)?
Ndiyo. Bidhaa zetu zinafaa kwa nywele za asili, nywele zenye dawa (relaxed), nywele zilizopakwa rangi na hata zilizosukwa. Zinalenga kuweka nywele zenye afya na kupunguza kukatika.


6. Nioshe nywele mara ngapi?
Tunashauri kuosha nywele mara moja kwa wiki au kila baada ya wiki mbili, kutegemeana na hali ya nywele zako na shughuli unazofanya.

Kati ya siku za kuosha, tumia Hair Growth Spray kila siku kuongeza unyevu.


7. Nitapata matokeo baada ya muda gani?
Matokeo hutofautiana kati ya mtu na mtu.

Wateja wengi huanza kuona nywele kuwa laini, zenye unyevu na kupungua kwa kukatika ndani ya wiki chache wanapotumia bidhaa kwa usahihi na kufuata routine.

Afya ya nywele ni safari, hivyo matumizi ya mara kwa mara ndiyo huleta matokeo bora.


8. Bei za bidhaa za ESN ni zipi?
🧼 Foaming Nourish Shampoo (400ml) – TSh 20,000

🧴 Deep Nourish Conditioner (250ml) – TSh 20,000

πŸ’§ Ultra-Moisture Leave-In Conditioner (200ml) – TSh 15,000

🌿 Hair Growth Oil (150ml) – TSh 20,000

πŸ’¦ Hair Growth Spray (250ml) – TSh 15,000

πŸ₯‘ Hair Nourish Butter (250ml) – TSh 20,000


9. Mnapatikana wapi?
Unaweza kuagiza popote ulipo Tanzania.

πŸ“ Bahari Beach, Dar es Salaam

πŸ“ Mikocheni Plaza, Dar es Salaam

Tunatuma bidhaa nchi nzima kupitia huduma za usafirishaji.

πŸ“ž Simu/WhatsApp: 0786 070 378


10. Nitawezaje kujua bidhaa zinazofaa kwa nywele zangu?
Tuma ujumbe WhatsApp au Instagram ukiambatanisha picha ya nywele zako na utuambie changamoto unayokutana nayo.

Tutakushauri routine inayokufaa bila malipo.

πŸ“ž WhatsApp: 0786 070 378